Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa mechi yao ijayo ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United haitokuwa nyepesi kwakuwa timu hiyo inakikosi kizuri.
Manara ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiwataka wapenzi wa klabu ya Simba kuiombea timu hiyo iweze kuibuka na alama tatu muhimu.
Kuhusu mechi ijayo…. baada ya kupona majeraha yake Emmanuel Okwi aanza mazoezi leo mjini Morogoro….Mechi ijayo dhidi ya Singida sio nyepesi,tunawaheshimu na tunajua wana team nzuri lakini Inshaallah tutapata matokeo mazuri..Dua na Sala zenu wanasimba wote
Kuelekea katika mchezo huo unao tarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi ya Januari 18, mshambuliaji wao hatari wa Uganda tayari hapo jana amejiunga na kikosi na kuanza mazoezi baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa muda.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: