MBUNGE wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amemuonesha Naibu wa Waziri wa Nishati, Subira Mgalau maeneo yenye mahitaji maalumu ya kupatiwa nishati ya umeme.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Talawanda akiwa ameongozana na Waziri wa Nishati, Subira Mgalau, Ridhiwani ametumia nafasi hiyo kuomba umeme na hasa katika hospitali kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa akina mama wajazito na watoto.
Pia amemsisitiza umeme uwekwe kwenye shule ili kuwapa nafasi wanafunzi wa Kata ya Talawanda na Chalinze kwa ujumla kujisomea wakati wowote.
"Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, moja ya changamoto iliyopo jimboni kwetu na hapa katika Kata ya Talawanda ni zahanati yetu kutokuwa na umeme, hivyo tunaomba mtusaidie na pia katika shule.
"Hivyo ukitusaidia kwenye changamoto hii utakuwa umetusaidia wananchi wa Chalinze, kukosekana kwa umeme inafanya hata huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto kuwa ngumu,"amesema Ridhiwani.
Ridhiwani amesema amefarijika kwani Naibu Waziri Mgalu ameahidi kusaidia kuleta umeme na katika mpango wa umeme wa miji inayokuwa kwa haraka Kata ya Talawanda ipo.
" Kwa zahanati zote zitaungwa umeme na hii italeta unafuu wa kupata huduma za afya katika jimbo letu, "
Kwa upande wake Mgalu amemhakikishi Mbunge huyo wa Chalinze kuwa Serikali inatambua umuhimu wa nishati ya umeme kwa wananchi na hivyo watapeleka umeme katika maeneo tote muhimu yakiwamo ya hospitali na shule kupitia mipango mbalimbali iliyopo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwasalimia wananchi wa kata ya Talawanda.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete(kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu walipokuwa Kata ya Talawanda jimboni Chalinze kwa lengo la kuzungumza na wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalau(wa pili kulia) akizungumza na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwa katika Kata ya Talawanda
Post A Comment: