Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kutembelea wananchi katika kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze.

Katika ziara hiyo amesikiliza kero za wananchi na kuzijadili kwa pamoja ili kupata muelekeo mzuri wa jinsi ya kuzitatua  na kati ya kero hizo kubwa ni pamoja na mahitaji ya Umeme ,Ajira kwa Vijana, maendeleo ya Afya,Elimu , Miundombinu na mengineyo.


Mh Mbunge  ametembelea kikundi cha maendeleo kinachojulikana kama JIPE MOYO  ambacho ni moja kati ya vikundi vilivyofaidika na fursa za Mitaji Katika Halmashauri na  Mfuko wa Jimbo  ambao upo chini ya Mbunge wa Chalinze
Share To:

msumbanews

Post A Comment: