Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe. John W. Heche, Ijumaa ya jana januari 12, 2018 amekabidhi mabati 50 kwa wananchi wa vijiji vya Kubiterere Kitongoji cha Nyansisine Kata ya Mwema,na badaye kwenda Kata ya Mbogi Kijiji cha Getenga na kukabidhi Mabati mengine 50 kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa shule ya Msingi .

Mbunge huyo pia ametoa mabati mengine  50 kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Borega B.

Aidha Heche amewashukuru na kuwapongeza wananchi kwa jitihada kubwa wanazozifanya kwa kuendelea na Maendeleo huku akiwaeleza Kuwa yeye kupitia Mfuko wa jimbo ataendelea kutoa vifaa vya Ujenzi ili kuwasadia wananchi hao kuwatia nguvu kuezeka Maboma yao waliyoyajenga.

Heche pia aliwambia wananchi Kuwa Halmashauri yake Kupitia Mapato yake ya Ndani kwa Mwaka huu Imepeleka zaidi ya  Milioni Mia tatu na Ishirini (320m) ili kuongeza nguvu kwa Wananchi kuezeka Maboma yaliyokaa zaidi ya miaka mingi.

Katika hatua nyingine, Baadhi ya viongozi na wananchi wamemshukuru Mbunge huyo na kuipongeza Halmashauri ya Tarime vijijini kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Mhe. Heche akiongea na wananchi jimboni kwake

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Mbunge, Mrimi Zablon, leo Jumamosi Januari 13, 2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: