Wakati unaendesha gari kwa mwendo ambao utakuruhusu kusimama katika umbali unaouona unafaa. Iwapo utashusha taa zako (yaani kuzifanya zimulike chini), au kumulikwa na taa za magari yanayokuja lazima upunguze mwendo – mbele gizani kunaweza kuwa gari bovu au mwendesha baiskeli.
Washa taa wakati wa usiku
Lazima utumie taa usiku (kuanzia nusu saa kabla ya jua kuchwa hadi kuchomoza) au mchana ambapo ni vigumu kuona kwa sababu ya moshi,ukungu, mavunde au mvua kubwa. Kwa mwongozo wa jumla washa taa zako unapokuwa huwezi kuona vizuri kwa zaidi ya mita 100. Usichelewe kuziwasha zinakufanya uonekane zaidi na wengine.
Kagua kama taa za gari lako ni safi na angavu
Hakikisha kuwa zinafanya kazi na zimerekebishwa vizuri. Taa lazima ziwekwe kiusahihi ili zitoe mwanga wa kawaida bila ya kuwaathiri madereva wengine fundi wa magari mwenye ujuzi anaweza kukusaidia kuangalia.
Tumia taa za mwanga mdogo unapolipita gari jingine (dim lights)
Washa taa za chini katika gari ili kuweza kuona wakati magari yanakuja mbele yako,wakati unaendesha nyuma ya gari au unalipita gari jingine.Wakati unaendesha mijini ambako kuna mwanga wa kutosha mtaani.
Usiwashe taa za ukungu (fog Lights) kama hakuna ukungu
Epuka kuwasha taa za mavunde au taa nyingine isipokuwa kama kuna mavunde sana au ukungu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: