Wapo wanawake ambao wamekuwa kwenye uhusiano kwa nyakati tofauti na na wanaume tofauti na kuishia kuachwa. Marafiki ukweli ni kwamba hakuna kanuni za moja kwa moja kwenye uhusiano, lakini angalau nivyema kuwa na uelewa wa mambo ya msingi zaidi kuyafahamu ili kujipa uhakika wa ndoa na boyfrend wako.
Wasichana wanaoachwa wengi wao hujitathmini sana lakini hawaoni kasoro iliyowaahanisha na wapenszi wao ambao awali walikuwa wakitangaza nia ya kuwaoa mara kwa mara.
Inawezekana yapo mambo mengi zaidi, lakini mambo haya hapa chini, ukiwa nayo makini, unajisogeza kwenye uhakika wa kuingia kwenye ndoa na boyfriend wako.
Kumkosoa sana
Baadhi ya wananwake wana kasumba hii. Boyfriend wake huenda anazungumza jambo au anachangia hoja fulani, yeye anamkosoa. Mbaya zaidi ukosoaji wke ni ule wa ujuaji, wenye kauli za kutojali na kuonyesha ujuaji zaidi. Bahati mbaya wananume kwa namna walivyoumbwa, kihulka hawapo tayari kuwa chini ya wanawake na hawajisikii vizuri kuonekana hawajui. Acha tabia ya kumkosoa mpenzi wako hata kama una uhakika kuwa anachosema si sahihi.
Lakini kwa uhusiano mzuri, wenye urafiki, zipo njia nzuri za heshima za kumkosoa mpenzi wako kwa hoja na siyo kumuonyesha kuwa ‘yeye si lolote’ bali hana elimu au uelewa wa jambo hilo. Mfano unaweza kumwambia, ‘Baby lakini ujue unavyosema si sawa, lakini kwa ninavyojua mimi…’, kwa lugha nzuri kama hii, mwanaume wako atakuwa tayari kukusikiliza na hutakuwa umemjeruhi hisia zake kwa kukuonyesha kuwa hana uelewa wa mambo.
Kuwa mkali
inawezekana mna mjadala fulani, zuia hisia zako na kuwa mkali, hasa kukaripiana. Mwanamke anapaswa kuwa mnyenyekevu kwa mwanaume wake. Kitndo cha kuonyesha ukali kwa boyfriend wako, kitampa taswira kuwa hata kwenye ndoa mnayoiendea, kelele na kumshushia heshima ndipo kutakapotawala uhusiano wenu, jambo ambalo litamfanya aondoe kichwani wazo la kufunga ndoa nawe.
Kumlinganisha na wanaume wengine
Epuka kabisa kumlinganisha mwanaume wako na wanaume wengine. wapo baadhi ya wanawake wana hulka hiyo. Wanapokuwa kwenye mijadala fulani au kuelekezana kitu kinachohusu majukumu yao, hulinganisha. Hilo ni kosa kubwa sana.
Utamsikia mwanamke anasema ‘Jifunze kwa wanaume wenzako, ona Jumanne anavyofanya kwa mpenzi wake Mayasa’. Kufanya hivyo ni kumuumiza mpenzi wako, lakini pia kutapunguza mapenzi na mawazo ya kukuoa. Mwanaume anapenda kuwa halisi, wa kipekee na asiyelinganishwa na yeyote. Mwanaume huamini alivyo, yupo tofauti na mwanaume mwingine yeyote kwa kila kitu, kumlinganisha ni kumfukuza mikononi mwako.
Usikubali faragha
Wanawake wengi hawajaelewa hii, lakini ukweli ni kwamba ili kumpa mwanaume mshawasha wa kukuoa jiweke mbali na mazingira yatakayorahisiha kukutana kimwili. Ni vizuri zaidi ikiwa kwenye uhusiano wenu kati ya ahadi muhimu iwe na ya kukutana kimwili mtakapokuwa kwenye ndoa.
Mwanaume anaweza kusukumwa na kiu ya ngono tu, lakini akishakupata huenda akakutana na vitu asivyotarajia na hapo ukawa mwisho wenu. Jiulize, utajaribiwa na wangapi? Kama mwanaume atafanya sababu ya kukataa kwako faragha kabla ya ndoa, kuhairisha ndoa na wewe, mruhusu aende salama kuliko kugeuzwa wa ‘mpira wa majaribio’. Msimamo wako utamfanya aone anakwenda kumuoa mwanamke mwenye heshima, anayejitunza na kuhifadhi maadili.
Kama bado unao usichana wako ni vizuri zaidi, lakini hata kama ulishafanya kosa, siyo mbaya kuanza kujilinda kwa upya ili meisho wa siku uingie kwenye ndoa ukiwa mpya kabisa kwa mumeo.
Acha kuomba sana pesa
Hili limekuwa tatizo kwa wanaume wengi. ni kweli mwanaume ana wajibu wa kumtunza mke wake, lakini asimgeuze mradi. Kwani kabla ya kuwa naye, ulikuwa unaishije? Ulikiwa huli? Hununui manukato nk? jibu ni hapana.
Jenga utaratibu wa kuvumilia ili akitaka kukusaidia fedha afanye yeye mwenyewe na siyo kwa shuruti zako. ukiendekeza pesa sana, atakupiga chini na kusubiri mwingine.
Mitindo isiyo na staha
Kwenda na wakati kumetaka kuharibu wasichana wa siku hizi. Kuna mavazi ya kubana au kuacha nusu ya sehemu ya mwili nje kwa kuamini ndiyo kuvutia – siyo kweli. Ukiona mwanaume anakusifia kwa mavazi yako ya hovyo, ujue hana nia ya kukuoa, anakutumia kama chombo chake cha starehe na siku ya kuoa ikifika, atamtafuta mwanamke mwenye maadili.
Usiwe hivyo, linda utamaduni wetu, heshimu uanawake wako kwa kuvaa mavazi ya heshima na kutengeneza nywele zako katika mtindo unaokubalika.
Post A Comment: