Mama mzazi wa muigizaji wa filamu hapa nchini, Irene Uwoya amefunguka na kueleza kuwa hamtambui mume wa sasa wa mwanaye, Dogo Janja na anachokijua yeye ni kuwa mume wa ndoa wa mwanaye amefariki mwaka jana.
Mama Uwoya ameongeza kuwa anachokifahamu yeye mpaka sasa mwanaye ni mjane, kwani aliyekuwa mume wake, Ndikumana amefariki dunia, na kabla ya hapo walikuwa wana ugomvi tu ila hawakuwahi kuachana.
Mama huyo aliendelea kueleza kuwa mwanaye, Irene uwoya, alifunga ndoa ya kanisani na aliyekuwa muewe, marehemu Ndikumana, ambaye walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume na walikuwa hawajaachana lakini walikuwa katika mgogoro ambao walishindwa kuutatua mpaka mwanasoka huyo alipopatwa na umauti.
“Ngoja nikwambie hakuna ndoa ambayo wazazi hawashirikishwi, ndoa yoyote lazima wazazi wajue na washiriki. Ninachojua kuwa irene ni mjane, mumewe ambae sisi tunamjua ndo huyo ameshafariki. Ninachojua mimi ni kuwa swala la ndoa lazima watu wazazi washirikishwe kuanzia mwanzo hadi mwisho,” alisema mama Uwoya.
Hata hivyo mama huyo anasema kwa kuwa kama Irene ni mtu mzima, basi anajua kitu anachofanya, hivyo hawawezi kumzuia na kumkataza. Lakini kitu cha kujua ni kwamba wazazi hawakuwahi kuapata taarifa kuwa mtoto wao alipewa talaka na mwanaume aliyefunga nae ndoa; na kwa sababu wao sio watu wa kufatilia vyombo vya habari hawakutaka kufatilia maswala ya media, ila walitaka kusikia kutoka kwa mtoto wao.
“Tunachojua mwanetu ni mjane, kama ana ndoa anaijua yeye. Lakini sisi hatuitambui na wala hatuaamini. Wala hatumjui huyo mtu anaitwa Dogo Janja labda wanaigiza,” alisema mama Uwoya
Post A Comment: