KOCHA mpya wa Simba, Pierre Lechantre kwa mara ya kwanza ameanza kukinoa kikosi hicho jioni ya leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuanza kwa programu za mazoezi, kikosi hicho kilichokuwa chini ya kocha msadizi, Masoud Djuma kilikusanyika  kwa pamoja na kuanza kumsikiliza Mfaransa huyo kwa takribani dakika kumi.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamehudhuria mazoezi hayo licha ya kuwa majeruhi ni kiungo, Haruna Niyonzima, kipa Said Mohammed 'Nduda' na beki, Salim Mbonde.
Majeruhi hao walijumuika na wachezaji wenzao kumsikiliza Mfaransa huyo kisha kukaa chonjo kutizama wenzao wanavyoendelea na mazoezi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: