Mahabusu ya watoto ya mkoa wa Arusha iliyojengwa miaka zaidi ya arobaini iliyopita inakabiliwa na changamoto  kubwa ya  uchakavu wa majengo pamoja na miundombinu mingine muhimu hali inayotishia hali ya afya ya watoto wanaohifadhiwa humo wakikabiliwa na makosa mbalimbali.

Msimamizi wa mahabusu hiyo Musa Mapua anaueleza ujumbe wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi waliowatembelea watoto hao kwa lengo la kuwapelekea mahitaji mbalimbali kuwa ubovu huo wa miondombinu ikiwemo ya maji safi na taka unatishia kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa watoto ikiwa ni moja ya maadhimisho ya miaka arobaini na moja ya kuzaliwa kwa CCM Diwani wa kata ya kati Abdi Tojo akawakumbusha wazazi jukumu lao la malezi ili kuwaepusha watoto kuishi kwenye mazingira hayo ambayo sio salama.

Mahabusu hiyo kwa sasa ina jumla ya watoto kumi na watano walioingizwa kwa makosa mbalimbali ambayo mengi yanaelezwa kuchangiwa na watoto kuachwa huru wakidhurura kujitafutia mahitaji hali ambayo Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo wa Arusha Godliving Kissila anasema wameweka utaratibu wa  kuanza kuidhibiti.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: