Zaidi ya Magari 500 yakiwemo ya kusafirisha abiria yanayotoka jijini Arusha, yamekwama kupita katika eneo la Makuyuni Mara baada ya Daraja linalojengwa kusombwa na maji yanayotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku Wa kuamkia Leo.

Taarifa zinadai kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha Leo majira ya SAA saba usiku na baadae maji yaliongezeka na kusomba Daraja hilo lililopo umbali Wa kilometa moja kutoka Makuyuni barabara ya MTO Wa mbu  wilayani Monduli .

Hadi sasa hakuna taarifa za maafa zilizoripotiwa kutokana na mvua hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: