Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga.
Madiwani 3 wa CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa nje ya kikao cha baraza la madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana na kujadili mkataba wa halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru ambayo inawanyanyasa wananchini
Madiwani hao ni pamoja na George Sanga diwani Kata Ramadhani, Sigrada Mligo, diwani viti maalum, Legnard Danda, diwani kata Ihungilo ambao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya Ihagara inayo kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa wananchi.
Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku kujadili suala hilo kwa madai kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo andikwa jina la kampuni hiyo.
"Ihagala kama nani? Tumewaambia sisi hatujamwajiri na baraza hili halijamwajiri huyo Ihagala hivyo sisi tunamjadili kama nani? Nimewaambia hayo mapendekezo yote wayapeleke kwa Mkurugenzi yeye ndiye mwajiri wa Ihagala" alisema Mwanzinga
Post A Comment: