BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Ngoma ya Sema, Hamadi Ally ‘Madee’ hatimaye amefungukia kile kinachodaiwa kuwa ni bifu zito lililopo kati yake na msanii mwenzake, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.
Akipiga stori na Mtandao huu , Madee alisema suala la uwepo wa bifu kati yake na Roma ni hisia tu zinazo-zushwa na mashabiki kutokana na vijembe wanavyo-tupiana na msanii huyo ambaye kimsingi ni mtani wake.
“Roma ni mtani wangu, mara nyingi huwa kuna masihara kati yangu na yeye, hata familia yake kwa ujumla, vile vijembe ambavyo huwa tunatupiana ule huwa ni utani tu hakuna uhalisia wowote, hatuna bifu kati yetu,” alisema Madee
Ally Katalambula
Post A Comment: