Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo yake na Rais John Magufuli yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam siku sita zilizopita.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Januari 15, 2015, Lowassa amesema alimueleza masuala mbalimbali yanayowakumba wananchi na wanasiasa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

“Nilijadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali ya msingi kuhusu nchi yetu ikiwemo kutoheshimiwa kwa Katiba na sheria, uminywaji wa demokrasia, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,” amesema na kuongeza,

“Unaohusisha kupotea kwa watu, kuvamiwa, kutishwa na kushambuliwa kwa viongozi wa kisiasa wa upinzani na hali ngumu ya uchumi kwa wananchi wetu. Ni imani yangu kwamba Rais atayazingatia na kufanyia kazi masuala haya kwa masilahi yetu.”

Kupitia barua hiyo, Lowassa amesema yupo madhubuti kuliko wakati mwingine wowote ule.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: