Utata huja pale unapokuwa unauliza kuhusu nani mwanasoka bora kuwahi kutokea wa kizazi cha vijana? Achana na Cristiano Ronaldo achana na Lioneil Messi lakini kuna kundi kubwa la vijana watakutajia Ronaldinho “Gaucho”.
Huyu huwezi kumuweka mbali na walipo kina Lioneil Messi an CR7 kwa kuwa Gaucho alikuwa kama jini wa soka, alionekana mtu ambaye alikuwa kama anaongea na mpira na kuuamrisha uende atakapo yeye.
Kaka wa Gaucho aitwaye Roberto Assis amethibitisha kwamba mwisho wa kaka yake kuutumikia mchezo wa soka umefika na sasa wao kama familia wanajipanga kufanya tukio la kumuaga Gaucho.
Assis amesema nchini kwao Brazil, Ulaya na Asia wamepanga kumfanyia jambo kubwa Ronaldinho Gaucho huku pia wakitafuta mpango wa ajili ya kufanya tukio hilo baadaye mwaka huu katika fainali za kombe la dunia.
Tayari makampuni kama Nike na pia klabu ya Barcelona ambayo Ronaldinho alikuwa balozi wao kwa miaka 10 sasa wako tayari kufanya tukio kubwa kwa ajili ya kumpa heshima mnyama huyo wa soka.
Post A Comment: