Priva ABIUD
Arsenal kwa Mara ya Tano wanakutana na Chelsea katika msimu mmoja. Hii ni kwa mara ya tatu inatokea ikiwa iliwahi kutokea mwaka 2003-04 na 1946-47). Mara hii ni marudiano katika mchezo wa Kombe la Carabao. Mchezo wa kwanza ulitoka sare ya bila nyavu kutikiswa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Taarifa za Timu
Taarifa za Timu
Chelsea
Itawakosa wachezaji wake muhimu kama Morata Alvaro pamoja na Fabregas Cesc waliopatwa na Majeraha. Kurejea kwa beki wao kati Andreas Christensen, pia Thibaut Courtois, Garry Cahil na Drinkwater Danny wote wapo fit.
Arsenal
Usajili mpya Henrik Mkhitaryan hatokuwepo katika mchezo huo kutokana na kuichezea Man United katika hatua ya mtoano. Watakao kuwa naa hati hati ya kutokuanza ni Aaron Ramsey (mgonjwa) na Nacho Monreal (maumivu ya mguu) lakini Olivier Giroud na Danny Welbeck hawa wataukosa kabisa mchezo huo.
Wachezani Muhimu
Kiwango Maradufu cha Jack Wilishere huenda kikawa tishio katika mchezo. Mesut Ozil ambaye inaonekana huenda akaongeza kandarasi yake. Hazard nae kuna uwezekano mkubwa akaanza kama mshambuliaji wa kati katika mchezo.
Takwimu.
*Chelsea haijafungwa mechi 12 za mwisho
*Arsenal ilivunja ukimya wa kutokushinda michezo mitano ya mwisho kwa kuifunga Brighton kwenye mchezo wao wa Mwisho.
*Vijana wa Antonio Conte wameonja kipigo Emirates mara moja katika mecho yote 8 katika uwanja huo
*Arsenal imeweza kufunga magoli 15 katika michezo mitatu ya mwisho ugani Emirates
*Chelsea katika michezo 4 ya mwisho wamepata wastani wa magoli manne katika kila mchezo.
Post A Comment: