Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.
Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha.
Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.
"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hadhi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea
Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi.
Post A Comment: