Ikiwa ni jana tu amekabidhiwa Timu kocha Mfaransa Pierre Lachantre raia wa Ufaransa mwenye uzoefu na soka la Afrika kutokana na kufundisha vilabu kadhaa barani Afrika na timu kadhaa za Taifa kocha huyo ameweka wazi vipaumbele vyake akiwa ndani ya Simba ili kuhakikisha timu inafanya vizuri ndani na Nje ya Nchi (Kimataifa)
Kocha Huyo ametaja vipaumbele vyake Vitatu kuwa ni Kuwa na Timu bora na Imara za Vijana, Nidhamu na Kuongeza Programu za Mazoezi ndani ya Simba.

Kuongeza Program za Mazoezi 

Kocha huyo amesema kuwa moja kati ya vitu vinavyofanya timu za Kiarabu kufanya vizuri ni kufanya sana mazoezi, Huku akisifia CV ya Kocha wa Mazoezi Aymen Mohammed kutokana na Kuwa amefanya kazi na Timu kama Esparance kwa muda mrefu hivyo kuwa yuko vizuri katika upande wa mazoezi.

Esparence ya Tunisia ni moja kati ya Timu kubwa barani Afrika kutokana na kufanya kwake vizuri kwenye michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika), Aymen amewahi kuwa mwalimu wa Viungo timu hiyo na sasa yupo Simba kumsaidia Pierre.

Nidhamu

Pierre amesema pia kuwa hakuna mafanikio bila Nidhamu ndani ya timu hivyo atahakikisha wachezaji wanakuwa na nidhamu kubwa katika kipindi chote atakachokaa Simba kama Kocha.

Kuwa na Timu za Vijana

Lechantre msomaji wa Msumbanews.co.tz amesema pia moja kati ya Vipaumbele vyake ni kuhakikisha Simba inakuwa na timu za Vijana kuanzia Umri wa Miaka 16, 19 na 21  moja kati ya Malengo hayo ni kuwa na timu yenye falsafa moja, Kupunguza Gharama za Kununua Wachezaji lakini Pia kuingiza Kipato kwenye Klabu kwa Kuuza Wachezaji hao wanapohitajika katika timu nyingine.

Simba kwasasa wanajiandaa na Mchezo dhidi ya Maji Maji mchezo unaotarajia kuchezwa katika uwanja wa Taifa na tayari Uongozi umetangaza Kuwa kocha Mpya Pamoja na Msaidizi wake leo wanatarajia kuanza kazi rasmi ndani ya Simba kwa kusimamia MAZOEZI ya Timu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment:

Back To Top