Mwendesha Mashitka wa Takukuru, Leornad Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameomba madaktari wake kutoka Afrika Kusini wawepo wakati akifanyiwa upasuaji wa puto.
Pia Swai ameeleza kuwa Mfanyabiashara James Rugemarila hana ugonjwa wa saratani, pia na yeye ameomba madaktari wake kutoka India wawepo wakati akiwa anafanyiwa uchunguzi.
Swai ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo upelelezi bado haujakamilika.
Wakili Swai alieleza kuwa taarifa kuhusu afya za washtakiwa alizipata magereza January 17, 2018 kama mahakama ilivyoamuru azifatilie.
Swai alidai mshtakiwa Sethi anaishi na puto tumboni ambalo limeisha muda wake, ambapo madaktari wa Muhimbili wamesema linatakiwa liondolewe.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema inaonekana madaktari wa Sethi wameruhusiwa kuja nchini kumtibia, hivyo Magereza wafanye utaratibu kama uliotumika kwa Sethi ili na Rugemarila atibiwe na madaktari wake.Kesi imeahirishwa hadi February 2,2018.
Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Post A Comment: