Huu ni Utabiri wa kikosi cha Yanga kinachoweza Kuanza dhidi ya Azam Fc katika Mchezo wa Raundi ya 15 Azam Complex saa 10 Alasiri.

Golini : Kutokana na Kuonekana kuaminiwa kwa muda sasa toka Ligi imeanza akicheza mechi zote za Ligi Youthe Rostand atakuwa golini bila shaka kama golikipa wa Yanga kwenye mchezo wa leo.

Mabeki wa Pembeni : Kutokana na ubora walionao Kwasasa Hassan Kessy upande wa Beki ya Kulia na Haji Mwinyi huenda wakaendelea Kuaminiwa kwenye mchezo wa Leo, Kessy msomaji wa Msumbanews.co.tz amekuwa na uwezo mkubwa wa Kuanzisha mashambulizi kutokea Kulia hukua akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza One Two na Kuingia kwa kasi lango la wapinzani licha ya Kuwa uwezo wake wa Kupiga Krosi bado si kama wa Juma Abdul.

Haji Mwinyi ambaye aling’ara zaidi CECAFA na Mapinduzi kiasi cha Kumpora namba Gadiel Michael naye amekuwa akimzidi Gadiel Uwezo wa Kupiga krosi zenye macho licha ya kuwa wote wanauwezo mzuri lakini kwenye mchezo wa Leo bado naiona nafasi ya Mwinyi Kuanza.

Mabeki wa Kati : Kurejea kwa Kelvin Yondani aliyekuwa akitumikia adhabu ya Kukosa mchezo mmoja ni wazi hakuna tena nafasi ya Makapu kucheza kama beki wa Mwisho, Ni wazi ataanza Yondani na Andrew Vicent “Dante” kama Mabeki wa Katikati.

Viungo wa Pembeni : Kutokana na kukosekana kwa Pius Buswita eneo la winga ya Kulia kocha anaweza Kumuanzisha Raphael Daud ili aweze kusaidia eneo la Katikati ya uwanja kutokana na uwezo wake wa Kucheza katikati ya Uwanja hivyo kusaidia viungo wa Kati na  Winga ya Kulia Emmanuel Martin huenda akaanza ili kuongeza kasi ya Mashambulizi.

Viungo wa Kati : Namba sita na Namba Nane huenda akaanza Makapu kama namba 6 akisaidiana na Papy Kabamba Tshishimbi kama namba nane, Au kama kocha akiamua kumtumia Tshishimbi kama namba 6 basi Makapu hatakuwa na nafasi ya Kucheza kwenye kikosi cha Mwanzo na huenda Raphael Daud akasogea namaba nane na Namba saba akaanza kati ya Said Mussa au Akilimali ambaye amerejea Kikosini.

Washambuliaji : Namba 10 ni wazi ataanza Ibrahim Ajib na Namba 9 Obrey Chirwa ambaye adhabu yake imeisha na leo anatarajia kurejea kwenye kikosi cha Mabingwa watetezi wa VPL Yanga. Kwa Kikosi kamili cha Yanga ungana nasi baadaye kitakapotoka, 

Kumbuka Kulike Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini

Share To:

msumbanews

Post A Comment: