Vituo vya Citizen TV na Citizen Radio vimezimwa na serikali nchini humo tukio ambalo limehusishwa moja kwa moja na kurushwa kwa matangazo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.
Citizen TV na Radio walikuwa wakirusha Live tukio la kuapishwa kwa Raila Odinga katika viwanja vya Uhuru jijini Nairobi.
Kupitia tovuti ya Citizen TV imeeleza kuwa tukio hilo limekuja siku moja baada ya Serikali kupitia Mamalaka ya Mawasiliano nchini humo (The Communications Authority of Kenya) kutoa onyo kwa vyombo vya habari vitakavyorusha matangazo ya kuapishwa kwa Odinga.
Post A Comment: