Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Allan Kijazi akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyofanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga.
Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa, Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kemilembe Lwota akitembea juu ya daraja hilo.
\
Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete naye hakua nyuma kutembea juu ya daraja hilo ambalo limeongeza shughuli za utalii kwenye hifadhi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa juu ya daraja maalumu lililojengwa kuwawezesha watalii kuwaona wanyama aina ya Viboko na aina mbalimbali za ndege.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akifurahia mandhari ya daraja linalomwezesha mtalii kuona vizuri eneo la Ziwa Manyara.
Post A Comment: