Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na waandishi wa habari na baaadhi ya wakuu wa idara mbali mbali pamoja na kati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo wakati alipokuwa akielezea mikakati ya Mkoa huo na shughuli ambazo zimefanyika.
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo.
Serikali mkoani Geita imetangaza oparesheni ya kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba hadi sasa bado awajawapelekwa shuleni na pindi watakapobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa seekondari hali sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa kuingia kidato cha kwanza kwani hadi sasa asilimia 46 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni.
Luhumbi ameongezea kwamba suala la elimu ni haki ya mtoto na hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri kwenye shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa kwenda shule na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.
Ameendelea kusema anafuatilia taarifa ya walimu ambao wameonekana kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo wakibaini hatua kali zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule walimu wameendelea kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.
katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na asilimia 54 .
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha wilaya ya Bukombe walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620 sawa na asilimia 41, Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia 57,Geita mji walichaguliwa 4,286 walioripoti ni
2,751,sawa na asilimia 64 huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni 1,924 sawa na asilimia 64.
Halmashauri ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na asilimia 50, wilaya ya Nyanghwale 2,601 walioripoti ni 1,344 sawa na asilimia 52.
Post A Comment: