UONGOZI wa klabu hiyo umesema kwamba hautamchukulia hatua yoyote beki wake, Juma Nyoso anayedaiwa kumpiga shabiki hadi kuzirai, tukio lililotokea kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, alisema kitendo cha Nyoso kilitokana na hasira ambazo zilisababishwa na shabiki huyo kufanya vitendo vya kichokozi dhidi ya Nyoso, hivyo kama timu haiwezi kumpa adhabu yoyote kwa sababu alichokozwa.
“Hata wewe ungekasirika, ifike mahali mashabiki wawe na uelewa kuwa wachezaji nao ni binadamu na wana mioyo, huwezi kumkwaza mwenzako bila sababu halafu ukatarajia akuchekee, sishabikii yeye kumpiga lakini siwezi pia kusema amefanya utovu wa nidhamu kwa hali kama ile,” alisema Mecky.
Katika mchezo wa juzi dhidi ya Simba  ambao walishinda mabao 2-0, beki huyo anadaiwa kumshambulia shabiki mara baada ya mchezo kumalizika ambaye alipata jeraha usoni, ambapo Nyoso alishikiliwa kwa muda katika kituo kikuu cha polisi, mjini Bukoba, ambapo kwa sasa yupo nje kwa dhamana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: