Wakati tukielekea katika chaguzi ndogo mbalimbali hasa katika Jimbo la Kinondoni na Siha zinazotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu, ni vyema wananchi wakafahamu majukumu ya msingi ya mbunge, ili waweze kumpima kama anayegombea anaweza kuyatimiza kisha wachukuea uamuzi wa kipiga kura.
Mbali na ahadi ambazo mgombea ubunge anaweza akaahidi, kuna majukumu yake ya msingi, hata asipoahidi lakini kutokana na kuchaguliwa tu, ni lazima ayatekeleze. Mfano, kujadili na kupitisha bajeti, hili lipo kisheria, japo haimaanishi kwamba mgombea ubunge haweza kulitumia katika kampeni
Kuna majukumu mbalimbali ya Mbunge lakini hapa chini tumeorodhesha majukumu sita, ambayo kwa kiasi kikubwa yanashabihiana. Mjukumu hayo ni;
  1. Kuwawakilisha wananchi wake bungeni katika masuala yote yenye masilahi yao mfano katika masuala ya afya, elimu.
  2. Kuwa kiungo kati ya Serikali na wananchi katika masuala yote ya maendeleo (kisiasa, kiuchumi na kijamii)
  3. Kutunga sheria mpya za nchi kupitia vikao vya Bunge
  4. Kuisimamia na kuishauri Serikali katika utendaji wake wa kazi
  5. Kujadili na kupitisha bajeti ya serikali yenye tija kwa wananchi
  6. Kulinda na kutetea masilahi ya ilani ya chama chake bungeni. (Jukumu hili kuna wakati linazua utata hasa pale ambapo maslahi ya chama yanakuwa sio maslahi ya umma).
Mbali na majukumu hayo, Mbunge anawajibu katika mambo mengine, kama vile kuwaheshimu na kuwathamini wananchi anaowawakilisha, kushirikiana na viongozi wengine (Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Madiwani) katika halmashauri ambayo jimbo lake lipo lakini pia kuwa mwaminifu kwa wananchi wake.
Mara nyingi wananchi wamekuwa wakichagua mtu kwa vile wanamfahamu, wanatoka chama kimoja, au ameahidiwa vitu ambavyo ilikuwa ni haki yake kuvipata licha ya kuwa ameahidiwa ama la, hivyo ni vyema kwa wananchi kuwa na elimu ya uraia ili waweze kupambanu mambo kwa mapana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: