Na Jerry C. Muro
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christina Mndeme akiwa ameshika moja ya gunia la serikali yaliyokamatwa kwenye ghala binafsi la Lotary Nkondola eneo la Ruhuwiko Songea.
Tukio hili limetokea Leo asubuhi kufuatia ziara ya ghafla NFRA kanda ya Songea kufuatia tuhuma za watumishi wa *NFRA* kuiba mahindi tani 30 toka maghala ya serikali hapo Desemba 2017.
Katika Picha wa kwanza kulia ni Meneja wa NFRA Songea Amos Mtafya (mwenye shati la drafti) na katikati ni Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema.
Kwenye tukio hilo mkuu wa Mkoa Mhe Mndeme ameagiza kukamtwa kwa meneja huyo pamoja na watumishi wenzake Lugano Moses (Mhasibu) na Mariam Mpangala ( Afisa Maghala) pamoja na wafanyakazi wa ghala binafsi wanne.
Post A Comment: