Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi(MUWSA) inazidai taasisi za umma  zaidi ya Sh 1.8 bilioni ikiwa ni malimbikizo ya ankara za maji zilizoishia Desemba mwaka jana huku jeshi la polisi likiwa kinara wa deni hilo.

Akitoa takwimu za wadaiwa hao leo Jumatano, mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Joyce Msiru amesema deni hilo ni hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana huku akilipongeza jeshi la magereza kwa hatua yao ya kuamua kupunguza hadi kufikia Sh 271.9 milioni.

Msiru aliitaja Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro kuwa inaongoza kwa kudaiwa kiasi cha Sh 876.3 milioni  wakifuatiwa na Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi(CCP) ambao wanadaiwa Sh 620.3 milioni.

Yaani madeni tunayoyadai kwenye taasisi za Serikali kama tungelipwa hizo fedha tungeweza kutoa huduma katika maeneo mengine nje ya Manispaa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za mamlaka yetu," amesema Msiru.

Akizungumzia kuhusu kudaiwa fedha hizo, Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, Hamis Issa alikiri kuwapo kwa deni hilo na kusema kuwa yeye hawezi kujibu chochote

Hilo deni kweli lipo ila mimi ni msimamizi wa mkoa na siwezi kulizungumzia kwa kuwa ni deni la jeshi la polisi na siyo deni langu kama Hamis Issa," amesema kamanda huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: