Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro,akiwa katika Picha Na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na baadhi ya Wafanyabiashara Mkoa wa Arusha. IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya siku mbili kwa ajili ya Ukaguzi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari zinazojengwa baada ya ajali ya janga la Moto lililotokea mwezi septemba 2017.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa Na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa walipotembelea Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari zinazojengwa baada ya ajali ya janga la Moto lililotokea mwezi septemba 2017.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro,akiwa katika Picha Na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa Nje ya Kituo kipya Cha Polisi Maalumu kwa ajili ya Watalii. IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya siku mbili kwa ajili ya Ukaguzi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari zinazojengwa baada ya ajali ya janga la Moto lililotokea mwezi septemba 2017.

Na Rashid Nchimbi


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewasili  mkoani hapa kwa lengo la kukagua Ujenzi wa Nyumba zinazojengwa kutokana na janga la moto lililotokea katika Kambi ya Polisi (new line) tarehe 27.09.2017 na kuteketeza Nyumba za familia 13 na kuridhishwa na hatua zilipofikia.

Katika ziara yake amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli  kwa kutoa Kiasi cha Tsh. Milioni 260 kujenga nyumba kwa ajili ya Makazi ya Askari yaliyoteketea kwa moto, ambapo Ujenzi wa Nyumba izo upo katika hatua za Mwisho kukamilika.
Pia ametoa shukrani Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kwa kuitisha Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha ambao kwa umoja wao walimuunga Mkono Mheshiwa Raisi kwa kujenga Nyumba kumi na nane (18). IGP Siro amewashukuru Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwa Umoja waliounesha kwa kufanikisha Ujenzi wa Nyumba izo.
Aidha amewataka Askari kutimiza wajibu wao na kutenda haki wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha uhalifu unapungua ili watu wafanye biashara kwa amani na kuendelea kujenga imani na Jeshi la Polisi ili waendelee kutoa ushirikiano na  kutoa msaada.

IGP Siro pamoja na Kamati ya Ulinzi wa Mkoa walitembelea ujenzi wa Vitu viwili vya Polisi. Kituo cha Polisi Muriet pamoja na Kituo cha Polisi Maalamu kwa Ajili ya watalii. Vituo vyote viwili vimejengwa kwa kwa ufadhili   
Mkuu wa mkoa wa Arusha ametoa Shukrani kwa Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha Tshs. Milioni 260 ambazo zimejenga Nyumba kumi na tatu 13 kwa ajili ya Makazi ya Askari.
Pia amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kuja kwa haraka kuangalia changamoto na madhara  yaliyowakumbuka Askari kutokana na Ajali ya moto. Aidha amempongeza Kamanda wa Polisi mkoa Arusha DCP Charles Mkumbo ambaye alikua mwenyekiti wa Ujenzi pamoja na Kamati ya Usalama wa Mkoa kwa kusimamia Vizuri ujenzi wa Nyumba izo.
Mkuu wa Mkoa pia amewashukuru Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwa kutoa Ushirikiano kwa Serikali katika dharura ya Ajali ya Moto kwa Ujenzi wa Nyumba 18.  

Share To:

msumbanews

Post A Comment: