Muigizaji wa filamu ambaye siku  zijazo anatarajia kwenda kuigiza katika filamu ya ‘The Blue Maurtius’ Idris Sultan, ametoa neno kwa Watanzania kuhusiana na majirani zetu Kenya kupata nafasi katika tuzo za filamu za Oscar.

Idris ametoa maneno katika mtandao wa Twitter na huku akionyeshwa kukerwa na baadhi ya watu wanaopenda umbea kuliko kazi.

“Kenya imepata Oscar award moja ya Lupita, imekua nominated Oscar award nyingine movie ya WATU WOTE na sasa wamefanikiwa kutengeneza satellite yao ya kwanza. Kwa kifupi watafanya yote ila hawatakaa watukute kwa instagram followers, sisi ndio noma. Satellite ndo nini ? Ina umbea ?,” ameandika Idris.

Washiriki wa tuzo za Oscar mwaka 2018 walitajwa hapo jana huku upande wa Afrika Mashariki imetoa filamu moja iitwayo iiywayo ‘Watu Wote/All of Us’ kutoka Kenya ambayo inazungumzia shambulizi la kigaidi la Al-shabaab lililotokea nchini Kenya mwaka 2014 katika eneo la Mandera ambapo watu 28 waliuawa kwenye tukio hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: