Juma lililopita, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema kwamba anataka wahamiaji wanaoingia Marekani wawe wametoka nchini Norway badala ya nchi za Afrika alizoziita tundu la choo (shithole). Katika mkutano wa kiuchumi unaoendelea nchini Norway, Trump ataweza kujionea kwanini wahamiaji wanaoingia Marekani hawawezi kutokea Norway.

Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Dunia (WEF), Norway ndiyo nchi bora zaidi kwa binadamu kuishi duniani. Wachunguzi kutoka katika jukwaa hilo wametoa tuzo hiyo kwa Norway baada ya kufanya uchunguzi ambao haukuhusisha tu ukuaji wa uchumi (pato la taifa), lakini pia hali ya maisha ya wananchi.
Wachunguzi hao walilazimika kupiga hatua ya ziada na kuangalia maisha ya wananchi kwa sababu, unaweza ukawa na uchumi unaokuwa vizuri na uwepo wa viwanda, lakini maisha ya wananchi yakawa yanaathirika kwa kiasi kikubwa na shughuli hizo mfano uchafu kutoka kwenye viwanda na kufanya wananchi waugue.
Wafanyabiashara kwa upande wao wanaamini kwamba, kukua kwa uchumi ndio kipimo bora zaidi cha kupima ubora wa maisha ya wananchi, kwa sababu ukuaji huo unamgusa kila mwananchi. Lakini wachambuzi hao walipinga kauli hiyo na kutolea mfano Marekani ambayo uchumi wake umekuwa ukikua lakini kuna tabaka la watu bado wamo katika umasikini.
Katika mkutano wa uchumi unaoendelea Davos nchini Norway, WEF wamewatahadharisha wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa kutokuamini kwamba ukuaji wa uchumi ndio suluhusho la matatizo ya kijamii.
WEF imetoa wito kwa nchi mbalimbali kuangalia vitu vingine kama kipato cha mtu binafsi, utofauti wa walionacho na wasionacho katika jamii, ujumuishi wa wananchi, ukuaji na maendeleo, uchafuzi wa mazingira, madeni, umasikini, pale wanapotaka kupima kama nchi imeendelea ama la.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: