Shirikisho la Vyama Vya wafanyakazi Nchini, TUCTA, limetangaza kwamba, hatma kuhusu kulipwa kifuta jasho kwa wafanyakazi walioondolewa kwenye utumishi kwa vyeti feki itatolewa kati ya mwezi  Machi na Aprili mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo na  Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa, ambaye amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya uongozi wa shirikisho hilo kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika hatua nyingine, Msigwa amesema, TUCTA imepokea rasimu ya awali ya sheria kutoka serikalini, kuhusu uunganishwaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, ili kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko hiyo pamoja na usumbufu wa utoaji huduma kwa wateja.
Aidha katibu huyo amefafanua kwamba shirikisho linaendelea kuipitia rasimu hiyo ili kubaini mapungufu na kutoa mapendekezo yao ili kuboresha sheria hiyo kabla haijapitishwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: