Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo wamesaini mkataba wa ushirikiano wenye lengo la kuisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kufuatilia na kudhibiti uvamizi wa viwavi jeshi hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo mkoani Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, amesema makubaliano hayo yamekuja kwa wakati muafaka ambapo Serikali ilikuwa inachukua hatua mbali mbali kukabiliana na tatizo hilo.\

Mwakilishi Mkazi wa FAO, Fred Kafeero, amesema Shirika hilo limekuwa likifanya kazi pamoja na Serikali katika nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania kudhibiti athari inayosababishwa na viwavi jeshi hivyo.

Kupitia makubaliano hayo, FAO itatoa msaada wa kiutaalamu na kifedha wenye thamani ya Dola za Kimarekani 250,000 ambazo ni zaidi ya Tshs. Milioni 550 kuimarisha ufuatiliaji na kukuza uelewa kuhusu viwavi jeshi kwa mazao kabla na wakati wa misimu ya kilimo ijayo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: