CHAMA CHA MAPINDUZIHISTORIA YA CCM TANGUTANU NA ASP
Imetolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu zaTaifa, Mikoa na Wilaya. Inapatikana pia katika kitabu cha
 Sera za Msingi za CCM
Makao Makuu ya CCMDodoma, 2004
 
 
 2
HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP1.0 UTANGULIZI:1.1
 
Maelezo ya awali
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwakwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).Tendo hilo la kihistoria lilikuwa ni la kuendeleza utamaduni uliokuwa umeanza hukonyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la kujiimarisha katika mapambano. Kwamfano, ASP kwa upande wa Zanzibar ilitokana na kuungana kwa African Association(AA) na Shirazi Association (SA), tendo ambalo liliunganisha nguvu za wanyonge katikamapambano ya kuundoa usultani na utawala wa kikoloni wa Kiingereza. Kwa upandewa Tanzania Bara, TANU ilitokana na kujibadilisha kwa Tanganyika African Association(TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa.Kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961 na ule wa Zanzibarkupitia Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, kulifanya TANU na ASP viwevimekamilisha jukumu la ukombozi wa nchi hizi kutoka makucha ya ukoloni mkongwena usultani. Hata hivyo, vyama vya siasa hivi viliendelea kukabiliwa na majukumu yakuendeleza mapambano ya ukombozi katika Afrika na kote duniani; kujengaTanganyika na Zanzibar huru kiuchumi na kijamii na kuimarisha umoja na mshikamanowa kitaifa,Katika mazingira ya ubeberu duniani wakati huo na hali ya unyonge wa mataifa haya
machanga, yakielewa kuwa ‘umoja ni nguvu’, Tanganyika na Zanzibar zilibaini umuhimu
wa muungano, hivyo ziliamua kuungana tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huo ndiouliowezesha kuzaliwa kwa Tanzania. Chini ya Muungano huo, Tanzania iliendelea kuwana vyama vya siasa viwili, yaani TANU na ASP katika mazingira ya chama kimoja chasiasa. Vyama hivi vilitambua fika kwamba vinahitaji chombo madhubuti cha uongozikatika kutekeleza majukumu yake ya ukombozi kwa ukamilifu hivyo uamuzi ulifanywarasmi wa kuvunja TANU na ASP na kuundwa kwa Chama Cha Mapinduzi tarehe 5Februari, 1977.Katiba ya CCM, katika Azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa wa Pamoja wa TANU na ASPtarehe 21 January, 1977, inaeleza kuwa, (uk. 2-3),
 “...kwa kauli moja tunaamua na
kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African Union(TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari, 1977 na wakati huohuokuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika
mambo yote kwa mujibu wa Katiba.” 
 
Muungano wa TANU na ASP ndio uliowezesha CCM kuwa Chama chenye nguvu, imarana madhubuti, hivyo kuwa Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya juu wakuwaunganisha Watanzania. Aidha, CCM kimeweza kuwaongoza wananchi katika
 
 3
mapambano ya kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadilikombalimbali yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.CCM kimeendelea kupewa dhamana nawananchi ya kuunda serikali na kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wademokrasia ya chama kimoja hadi sasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi,kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya TanzaniaJuni 1992.1.2
Umuhimu wa kuielewa historia ya CCM na Vyama vilivyokitangulia
Historia ya CCM tangu TANU na ASP ina umuhimu wa pekee katika Taifa letu katikakuelewa tulikotoka, tulipo hivi sasa na tunakoelekea. Historia ya nchi yetu haiwezikukamilika bila ya historia ya vyama hivi vya ukombozi. Historia hutoa mafunzo na nimwelekezaji pia, kwa hiyo ni wajibu wa Watanzania, hasa wanachama wa CCMkujifunza kutokana na historia yetu. Kazi kubwa na ya msingi inayofanyika katikakujifunza historia hiyo, ni kurithisha dhamira ya kujituma na kudumisha uhuru wa nchiyetu. Hivyo, ili kuendelea kukijenga Chama, na kuimarisha uwezo wa kuendeleakukamata dola barabara kwa namna endelevu, hapana budi ihakikishwe kuwa historiaya CCM inabeba pia jukumu la msingi la kusaidia:-
 
Kujua Chama kilikotoka, mahali kilipo na kinakoelekea katika misingi ya sera,itikadi, malengo na wanachama.
 
Kuunganisha wanachama na kuwaweka pamoja kiimani, kiitikadi nakiutendaji.
 
Wanachama kujitambua, kutambua wajibu na majukumu yao na kujengamoyo wa kujiamini na kujithamini.
 
Kuinua kiwango cha ushiriki wa wanachama wa CCM na wananchi katikakubuni na kutekeleza mkakati na mbinu sahihi za kutetea na kuendelezaChama na taifa kufuatana na hali ya wakati na mahali.
 
Kuweka misingi ya kufanya tathmini na hivyo kuwa na uhakika katika kufanyamaamuzi.
 
Kupanda mbegu bora za upendo, uzalendo na uchungu wa kweli kwa uhai waCCM na taifa kwa ujumla.
 
Kuwa na majibu sahihi wakati wote kwa hoja mbalimbali zinazotolewa kuhusuChama Cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla.
 
Kuweka msingi wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine maadili yamsingi wa uhai wa CCM.
 
Kuhifadhi kuweka na kueneza kumbukumbu sahihi ya historia ya Chama,nchi, mchango wa Waasisi na wanachama na kuhakikisha wapotoshajihawapati fursa ya kueneza uongo.1.3
 Chimbuko la Historia ya CCM
Pamoja na kwamba Chama Cha Mapinduzi kuwa kilizaliwa rasmi tarehe 5 Februari,1977, chimbuko lake linaanzia miaka mingi kabla, sambamba na historia ya uhai wataifa la Tanzania. Mizizi ya historia ya CCM imo ndani ya harakati za kukataa ukoloni nausultani, zilizofanywa na wananchi wa Tanzania. Wahenga wetu kwa pamoja tanguenzi, walionyesha wazi kukataa kwao kutawaliwa. Historia ya Tanzania inao utajiri wa


Share To:

msumbanews

Post A Comment: