CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Manyara, kimekiri baadhi ya viongozi ndani ya chama walikuwa wanakihujumu kupitia mali zake, lakini wakati umefika sasa wa kurekebisha kasoro na kusonga mbele kwa maslahi ya umma.


Katibu wa CCM wa Mkoa, Paza Mwamlima, alisema hayo wakati akizungumza na Nipashe ofisini kwake namna ambavyo chama kimekwishaanza kuhakiki mali zake na kuchunguza watu ambao walikuwa wanajinufaisha kupitia mali za chama.

“Tumegundua wapangaji katika nyumba zetu walikuwa hawajapewa maelekezo sahihi na makatibu wetu wa matawi na kuwapa mikataba sahihi sasa tunaenda kuifumua na kuiunda upya ili kuondoa udanganyifu uliokuwapo,’’ alisema.
Aidha alisema makatibu wa matawi walikuwa wanatoa taarifa kuwa upangishaji wa vyumba katika nyumba za chama ni Sh. 15,000, lakini kwa kiuhalisia walikuwa wanakodisha  kwa Sh. 75,000 na kuzitumia fedha hizo.
Alisema kwa kasi ya uongozi wa sasa wa chama, kiongozi asiyekuwa mzalendo atatakiwa awapishe au chama kitamwondoa ili wengine ambao wanaweza kuwajibika waweze kuendelea kusimamia mali za chama na kuwaletea maendeleo wananchi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: