Msanii Bushoke amefunguka na kuwashauri wasanii Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) na kusema kuwa kwa sasa wanatakiwa kukitumia kipindi hichi vizuri ili kuweza kufanikiwa na kupiga hatua zaidi katika muziki.

Bushoke amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio kwenye Heshima ya Bongo fleva na kudai kuwa anaamini watu hao saizi wamechelewa kutokana na kukaa muda mrefu jela lakini kwa nafasi walionayo sasa wanaweza kufanya mambo makubwa kama wataitumia vizuri.

"Nawaombea watulie, watumie hii nafasi waliyopata sasa vizuri, naweza kusema wamechelewa lakini pia hawajachelewa kutokana na nafasi waliyonayo sasa najua watafanya makubwa sana" alisema Bushoke

Mbali na hilo Bushoke amesema toka wasanii hao wametoka jela na kurudi mtaani wamekuwa wakikutana na kufanya mazungumzo mara kwa mara lakini bado hawajakaa na kuzungumza juu ya wao kufanya kazi pamoja.

Bushoke ameiachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Goma la ukaye'
Share To:

msumbanews

Post A Comment: