Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.
Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.
Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.
Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.
"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"
Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana) , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.
Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.
Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.
"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.
Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.
Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.
Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.
"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.
Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.
Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha

Post A Comment: