Wakati Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiendelea  kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kupamba moto.

Mapema leo mchana Jan. 27, 2018, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM.

Madiwani ambao wamejiuzulu nyadhifa zao mapema leo asubuhi ni 
Juliana Malamsha,(Diwani Viti Maalum),  Marta Ushaki ( Diwani Viti Maalum) na Frank Joseph Umega(Kata ya kelamfua Mokala Mamlaka ya Mji Mkuu) wamejiuzulu udiwani wao na nafasi zao zote ndani ya Chadema  na wameomba kujiunga na CCM kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Rombo na Kikao cha chama kimewakubalia kujiunga na kuwapokea ndani ya CCM.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: