Mtuhumiwa.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Ami Lukule, anayedaiwa kuwaua mke na mtoto wake kichanga cha umri wa miezi minane na mdogo wake wa kike, katika eneo la Matosa Darajani, Goba wilaya ya Kinodnini jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita.
Akizungumza na wanahabari leo Januari 16, 2017 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumya Dar, Lazaro Mambosasa amemsema mtuhumiwa huyo alikamatwa hivi karibuni mkoani Iringa.
Waliouawa.
“Mtuhumiwa huyo tayari tumeshamkamata na baada ya kumhoji alikiri kufanya tukio hilo na kusema chanzo alikuwa mtoto. Amedai mkewe huyo alimtilia mashaka kwa kuingia kwenye mahusiano na mwanammme mwingine, anadai mke huyo alimzalia mtoto nje ya ndoa, hivyo akaamua kumnyonga mtoto na kufanya mauaji mengine mliyoyasikia,” alisema Mambosasa.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema kwa sasa wanafanya taratibu za kumsafirisha mtuhumiwa huyo kutoka Iringa hadi Dar ili kufikishwa mahakamani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: