Bodi ya ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) imefanya mabadiliko ya michezo miwili kutokana na sababu tofauti.
Mchezo wa kwanza ni baina ya Mbao FC dhidi ya Kagera Sugar uliyopangwa kufanyika tarehe 3 ya mwezi Februari katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, ambapo kwa sasa utafanyika Februari 4  katika uwanja huo huo huku sababu ikitajwa kuwa ni kutokana na uwanja huo kuwa na shughuli nyingine ya kijamii.
Mchezo wa pili ni kati ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar ambao awali ulikuwa umepangwa kupigwa Februari 7 mwaka huu, na sasa umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Februari 8, mwaka huu.
Wakati wa muzungumzo na waandishi wa habari bodi ya ligi imesema kuwa  sababu za mabadiliko hayo ni kuipa nafasi timu ya Kagera Sugar kusafiri na kupata nafasi ya kupumzika kwa kuwa mechi yao ya Februari 3 jijini Mwanza imesogezwa mbele kwa siku moja.
Mzungo wa pili wa ligi hiyo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi ya Feberuari 3 kwa michezo sita kupigwa kama ifuatavyo:-
Azam FC vs Ndanda FC,
Lipuli FC vs Yanga SC,
Singida United vs Mwadui FC,
Stand United vs Mtibwa Sugar,
Majimaji FC vs Mbeya City,
Tanzania Prisons vs Njombe Mji.

Jumapili kutakuwa na mechi mbili ambazo ni:-

Mbao FC vs Kagera Sugar,
Ruvu Shooting vs Simba SC.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: