Wafanya Biashara wa matunda Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa kwa sasa matunda yameongezeka, huku wakibainisha wazi bei ambazo wanauza kwa wateja wao. 

Wakizungumza leo na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam wafanyabiashara  hao kuhusu bei ya matunda sokoni hapo. Bei hizo ni kama ilivyo hapo chini.
Bei ya tikitiki maji ni kati ya Sh.1000 hadi Sh. 3500.
Bei ya Parachichi ni kati ya Sh.500 hadi Sh.1000.
 Bei ya Ndizi Mbivu inauzwa kati ya Sh. 100 hadi Sh. 160.
 Bei ya Embe sokoni hapo ni kati ya Sh.400 hadi Sh.700.Bei hiyo hiyo kwa wanaonunua kwa rejareja.
Bei ya Tango  katika Soko la Mabibo yanauzwa kwa fungu moja lenye matango matano kwash.1000.
Bei ya Ndizi inauzwa katika sokoni hapo inauzwa kati ya Sh.20000 hadi Sh.30000 kwa mkungu mmoja.
Bei ya viazi vitamu Sh.1000 kwa fungu katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wanunuzi na wauzaji katika soko hilo wakiwa katika pilikapilika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: