Dakika ya 7 tu Chelsea walionekana kama wanatangulia kwenda Wembley baada ya Eden Hazard kuwapatia bao la kuongoza hili likiwa ni bao lake la 4 katika mechi 6 zilizopita.
Lakini dakika 7 baadaye Antonio Rudiger alijifunga na Arsenal wakapata bao la kusawazisha na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa timu hizo kuwa sare ya moja moja.
Granit Xhaka alikuwa katika siku nzuri sana usiku wa jana na alipiga mashuti 3 langoni mwa goli la Chelsea na moja kati ya mashuti hayo ndio lilileta bao la pili la Chelsea.
Sasa Arsenal wanakwenda kukutana na Manchester City katika fainali ya michuano ya EFL na hii itakuwa fainali yao ya 8 ya michuano hiyo, ni Liverpool tu(12) na United (9) ndio wameshiriki fainali nyingi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: