WATU wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria kampuni ya Mkombozi kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Walawi katika eneo la Kamanga jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na abiria mwingine wamepoteza maisha papo hapo.
“Ni kweli imetokea ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili akiwepo dereva la basi dogo la Kampuni ya Mkombozi ambaye alifariki papo hapo na abiria mwingine, lakini pia wapo majeruhi watatu ambao wamepelekwa hospitali kwa matibabu zaidi,” alisema Msangi.
Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo za ajali hiyo.
Post A Comment: