Kanuni zinasemaje juu ya Tukio la Juma Nyosso? Hizi Hapa Kanuni ya 37 Ya udhibiti wa Wachezaji inasema mchezaji atakayesababisha na kufanya vurugu za aina yoyote na mara baada ya mchezo kumalizika atafungiwa kati ya michezo mitatu mpaka sita na faini ya shilingi laki 5.
Lakini mchezaji Juma Nyosso msomaji wa Msumbanews.co.tz anaweza pia kuhukumiwa kwa kanuni ya 10 inayosema
Mchezaji atakayebainika kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu yanayojirudia au mara nyingi (Sugu wa utovu wa nidhamu) atafungiwa kucheza kati ya michezo mitano mpaka kumi na faini isiyopungua milioni 1.
Hizo ndizo kanuni mbili ambazo zinaweza zikatoa Hukumu kwenye sakata la mchezaji Juma Said Nyosso baada ya kumpiga shabiki anayeaminika kuwa ni wa Simba anayedaiwa alimtolea Lugha za kumuudhi mchezaji Juma Nyosso mara baada ya Mchezo Kuisha.
Post A Comment: