Mheshimiwa Waziri wa Maji Engineer Kamwele leo ametembelea Mradi wa Maji wa Chalinze na kujionea maendeleo ya Mradi huo. Katika Ziara hiyo Mheshimiwa Waziri alifuatana na Mbunge wa Jimbo Ndg. Ridhiwani Kikwete, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga, Mwenyekiti wa Halmashauri na wataalamu mbalimbali.

Akizungumza na Waandiahi baada ya kutembelea Mradi , Mheshimiwa Waziri ameeleza masikitiko yako kwa kuchelewa kumalizika mradi huo.” Mradi huu ulikuwa uishe mwezi wa Pili mwaka huu 2017 , baada ya mjadiliano tukakubaliana kuwa itakapofika Octoba 2017 mradi uwe umekamilika, lakini la kushangaza pamoja na marekebisho hayo ya mkataba hadi leo nyie wenyewe mmeona hakuna lolote na nimejiridhisha kuwa hawawezi kazi hii tuliyowapa.” Pamoja na hayo Mh.Waziri aliwajulisha Viongozi aliofuatana nao kuwa wameshaanzisha utaratibu wa kuvunja Mkataba , ambao hadi tarehe 8 february mkataba utakuwa umekwisha. Hivyo kama wanataka mjadala wowote basi hadi kufika tarehe hiyo kazi iwe imefanyika.

Naye Mbunge wa Chalinze, alitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana Serikali kwa hatua kubwa walizozichukua kimkataba. Alimkumbusha Waziri kuwa Mradi huu ni wa Muda mrefu na ukipita kwenye Miundo Mbinu utaona hali ilivyo mbaya. Kazi inakwenda Taratibu sana na hakuna dalili ya wanachalinze kunywa maji safi na salama mapema mwakani. Alitumia nafasi hiyo pia kumuomba Waziri azidishe kasi ya usimamizi ili kabla ya Kipindi cha Pili Cha mwaka 2018 kazi iwe imekwisha maana watu wa Chalinze wamesubiri sana.

Mh. Waziri wa Maji alimuahidi Mbunge kuwa Serikali italisimamia hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: