Shilingi bilioni 3.1 zimetumika kujenga majengo ya chuo Uuguzi na Ukunga Mirembe mjini hapa ambayo yatasaidia kuongeza idadi ya wahitimu wa kada hiyo nchini
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa makabidhiano ya majengo hayo yaliyojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia  was Kupambana na UKIMWI,KiFUA KIKUU na Malaria(Global Fund)
Waziri Ummy mwalimu alisema anawashukuru Global fund kwa kusaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali nchininhasa katika mikoa kumi na saba ya Tanzania bara katika ujenzi wa vyuo,nyumba za watumishi ,maghala ya kuhifadhia dawa pamoja na magari ya kusafirishia dawa kupitia bohari ya dawa(MSD)
“Bila afya hakuna viwanda wala kilimo,hivyo serikali ya awamu ya tano imejikita katika utoaji wa huduma wa afya na rasiliamali watu na hivyo tunatarajia kuona ongezeko LA wanafunzi katika vyuo vyetu”
Aidha, Ummy alisema kupitia mfuko huo umesaidia nchi katika kukabiliana na UKIMWI,Kifua kikuu na Malaria
Alisema Watoto 10,000 nchini Tanzania huzaliwa wakiwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa Mwaka huku watu zaidi ya 900,000 wakitumia dawa za kufubaza Makali ya ugonjwa huo (ARVs).
Waziri alisema idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na wajawazito wanaobainika kuwa na VVU hivyo kunahitajika kazi ya ziada ili kukomesha kabisa tatizo hilo na watoto wazaliwe wakiwa wazima.
Umymy alisema serikali imejipanga kuona tatizo hilo linakwisha kwani inawezekana kabisa mtoto kuzaliwa bila ya maambukizi ya Ukimwi na hilo ndilo lengo lake akiwa Wizara ya afya.
“Hali ya maambukizi bado iko juu, kwa sasa tumeshasajili watu laki tisa ambao wanatumia dawa za kufubaza Makali ya Ukimwi na tatizo kubwa ni idadi ya watoto 10,000 ambao huzaliwa wakiwa na maambukizi, nataka tutoke huko,” alisema Mwalimu.
Waziri alisema wizara kwa sasa bajeti imeongeza kutoka asilimia 9.2 kwa Mwaka 2016/17 hadi kufikia asilimia 10 kwa Mwaka 2017/18 na kuifanya sekta ya afya kuwa sekta ya kipaumbele miongoni mwa sekta za kipaumbele katika mgao wa bajeti hivyo hakuna kisingizio tena.
Kuhusu vyuo vya uuguzi alikiri Wizara kuvisahau kutokana na taarifa ya mkuu wa chuo hicho Athanas Paul kwamba aliomba sh 300 milioni lakini kwa ajili ya shughuli za uendeshaji lakini tangu januari serikali ilipeleka chuoni hapo Sh 150,000 tu.
Alisisitiza Wizara kutupia macho katika eneo hilo ikiwemo kufuta jina la chuo cha Mirembe na badala yake kisomeke Dodoma Mirembe Nursing Collage kwani Mirembe ni hospitali ambayo wengi huamini kuwa walioko huko wanamagonjwa ya akili.
Katibu Mkuu Wizara ya afya Dk. Mpoki Ulisubisya alisema Chuo hicho kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa Watumishi ikiwemo Majengo kwa ajili ya ofisi na madarasa.
Ulisubisya alitaja uhaba wa Watumishi lakini akasema mambo hayo yatashughulikiwa kwa ukaribibu zaidi ikiwemo Majengo yaliyojengwa na Global Fund ambayo yanakwenda kupunguza msongamano huo.
Mwakilishi wa Global Fund Martha Setembo alisema ushirikiano wa mfuko huo na serikali ulianza Mwaka 2003 kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya.
Setembo alisema ziko fedha nyingi ambazo zimetengwa kwa ajili ya kusaidia sekta hiyo katika miradi inayotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo na akaomba serikali kuendelea kuitumia vema miradi hiyo ikiwemo Majengo wanayokabidhiwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Majengo ya vyuo vya uuguzi.
video


Kikundi cha Ngoma ya Mganda wa kabila la Wangoni wakionesha ubora wao wa kucheza mganda wakati wa tukio hilo la ufunguzi wa majengo hayo ya Chuo cha Uuguzi na Ukunga  Mirembe
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uuguzi na Ukunga Mirembe wakiimba wimbo wakati wa tukio hilo
Mkandarasi alojenga majengo ya chuo cha Uuguzi Mirembe,  Bwana Nishit Jethwa kutoka kampuni ya V.J. Mistry Co LTD ya Mkoani Kagera akizungumza katika tukio hilo
Mshauri elekezi wa mradi huo Dkt. Moses Ockony Mkurugenzi wa Mekon Arch Consult LTD akizungumza wakati wa tukio hilo
Mkuu wa chuo cha Uuguzi Mirembe,  Athanas Paul akisoma taarifa ya chuo hicho
Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika tukio hilo
Mwakilishi wa wizara ya fedha kamishna msaidizi,  Adrian Njau akitoa shukrani mara baada ya ufunguzi wa majengo hayo
 
Waziri Ummy Mwalimu akihutubia katika tukio hilo
Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo hilo, kulia ni mwakilishi toka Global Fund Martha Setembo, Afisa wa mradi huo kutoka wizara ya afya Dkt. Catherine Joachim (kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya
Waziri Ummy Mwalimu akisoma maandishi ya jiwe la ufunguzi wa jengo hilo, kulia ni mwakilishi toka Global Fund,  Martha Setembo
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wa mradi huo 
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  wawakilishi kutoka wizara yake pamoja na viongozi w Mkoa wa Dodoma 
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  wawakilishi kutoka hospitali hiyo ya Mirembe, Chuo hicho cha Uuguzi Mirembe 
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha Mirembe
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na afisa wa mradi huo kutoka wizara ya afya Dkt. Catherine Joachim (kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya
Jengo hilo linavyoonekana kwa nyuma
Sehemu ya jengo hilo linavyoonekana kwa mbele
Baadhi ya wanafunzi hao wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mirembe wakifurahia jambo wakati wa tukio hilo la uzinduzi wa majengo hayo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: