Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Viongozi na wajumbe wa bodi ya Chama cha Ushirika mkoa wa Mwanza Nyanza Cooperative Unioni (NCU) na Chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Region Cooperative Union - SHIRECU) kuandika maelezo na kuhusu mali za vyama vyao na kuziwasilisha katika ofisi ya Waziri mkuu Januari 13,2017.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo leo Desemba 22,2017 wakati wa kikao cha wadau wa pamba kutoka mikoa 16 nchini kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Savannah Plains mjini Shinyanga.
Mheshimiwa Majaliwa amesema mali za vyama hivyo hivi sasa zinamilikiwa na watu binafsi hivyo kutaka maelezo juu ya mali hizo.
Amewataka viongozi zaidi ya 10 wa Nyanza na wanne wa SHIRECU kuwasilisha katika ofisi ya waziri mkuu Dodoma nyaraka kuhusu mali zao na vyama vyao
“Nilitakiwa sasa hivi nimwambie kamanda wa polisi mkoa aondoke na nyinyi lakini tunataka taarifa zenu za awali kila mmoja aandike maelezo yanayojitosheleza kuhusu mali zinazomilikiwa na ushirika na sasa mali hizo ziko wapi na tarehe 13 mwezi Januari saa tatu na nusu asubuhi”,alieleza.
Viongozi hao wanadaiwa kufanya ubadhirifu na kuua ushirika na kulifanya zao la pamba kukosa thamani
Post A Comment: