Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemponza msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba kwa baadhi ya mashabiki zake ambao wameonesha kutopendezwa na msanii huyo kujihusisha na masuala ya kisiasa, baada ya Alikiba kuweka video ya Mkuu huyo wa mkoa.



Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii aliweka video ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisisitiza wananchi juu ya umuhimu wa  kulipa kodi na kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato.


Kitendo hicho alichofanya Alikiba kimewafanya baadhi ya mashabiki zake kuonesha kutofurahishwa huku wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka msanii huyo asijihusishe kabisaa na masuala ya siasa, japo wapo baadhi yao ambao hawakuona tatizo msanii huyo kuweka video hiyo. 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: