Kamati
ya Utendaji ya Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limemchagua
Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kuchukua nafasi ya
Patrobasi Katambi aliyehamia Chama cha Mapinduzi.
Kamati
hiyo pia leo Desemba 2 imetangaza kuziba nafasi ya nafasi ya Makamu
Mwenyekiti kwa kumteua John Pambalu, nafasi iliyoachwa wazi na Sosopi.
Viongozi hao wameteuliwa kuongoza baraza hilo kwa muda wa mwaka mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita amesema
uamuzi huo ulifanyika jana kufuatia kikao cha dharura cha kamati hiyo ya
utendaji.
Amesema
baraza hilo ni mojawapo ya taasisi imara na itaendeleza
mapambano."Tunawahimiza vijana wa Chadema na vijana wote wa Tanzania
wasimame kidete kwenye kazi ya kuijengea na kuipigania demokrasia ya
nchi yetu katika misingi ya utawala bora na haki za binadamu,"
Kwa
upande wake Ole Sosopi amesema katika uongozi wake atahakikisha baraza
hilo linarudi kwenye misingi imara na kuongoza mapambano ya kudai
demokrasia.
Amesema akiwa mwenyekiti hatavumilia kuendelea kuona uonevu wanaofanyiwa wanachama wa Chadema.
"Bavicha
inaenda kuwa taasisi bora na imara zaidi baada ya kuondoka Katambi.
Tunakwenda kupambania Demokrasia a, tutawashawishi vijana kuwa wamoja
kulitetea taifa bila kujali maslahi ya vyama," amesema Ole Sosopi
Post A Comment: