Wabunge nchini Uganda wamepitisha mabadiliko ya Katiba ambayo ya yametoa ukomo wa umri wa Rais kusalia madarakani ambapo awali ukomo ulikuwa ni miaka 75.

Kwa mabadiliko hayo yatamruhusu Rais wa sasa wa Uganda, Yoweri Museveni kuwania urais kwa muhula mwingine wa sita.

Kwa maana nyingine Rais Museveni ambaye alibakiwa na miaka miwili tu kufikisha miaka 75 na kuachia madaraka kwa sasa ataendelea kuongoza nchi hiyo hadi atakapoamua kuachia madaraka au kushindwa katika uchaguzi.

Baada ya majadiliano mazito na mivutano mikubwa Wabunge wa upinzani walitoka nje ya Bunge zaidi ya mara moja ambapo Wabunge sita kati yao walifukuzwa bungeni kutokana na kuupinga muswada huo.

Jana jioni Spika wa bunge hilo Bi. Rebecca Kadaga alitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.

Kwa upande mwingine, Wabunge wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka 7 hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: