Mlinzi wa kampuni ya Amspec, Mwajuma Ibrahimu amefariki dunia baada ya tani 9,500 za ngano kuporomoka ghalani na kumwangukia.


Ghala (silo) hilo lipo Kurasini jijini Dar es Salaam, mali ya kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL).


Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Bandari, Robert Mayala amesema leo Jumamosi Desemba 23,2017 kuwa tukio hilo lilitokea jana Ijumaa Desemba 22,2017 saa 10:00 alfajiri.


Amesema ghala hilo lilipasuka ndipo ngano ilipoporomoka hadi kwenye ofisi aliyokuwamo mlinzi huyo.


Amesema kazi ya kuondoa ngano ili kutoa mwili wa mlinzi huyo inaendelea.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: