Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa na Mbunge wa Arusha
mjini, Godbless Lema wameenda kwenye kituo cha polisi Usa River kutoa
taarifa ya tukio la uvamizi uliofanyika nyumbani Nassari usiku wa
kuamkia leo Jumamosi.
Tukio hilo limetokea Kijiji cha Nkwanekori wilayani Arumeru mkoa wa Arusha.
Katika ukurasa wake wa Twitter Nassari ameandika, “Nimevamiwa
nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na
kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba.
Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi.
Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.”
Baadhi ya majirani na viongozi wa Chadema wamefika nyumbani kwake
kumjulia hali na baadaye kumsindikiza kituo cha polisi Usa River.
Post A Comment: